RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Askofu Mkuu Wa TAG Awakanya Wachungaji Wanaoandikisha Viwanja Vya Makanisa Kwa Kutumia Majina Yao.


Askofu Mkuu Wa Kanisa La Tanzania Assemblies Of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali, Amewaonya Viongozi Wa Kanisa Hilo Wanaosajili Mali Za Kanisa Kwa Majina Yao Kuacha Mara Moja Maana Kufanya Hivyo Ni Sawa Na Wizi Na Ufisadi.



Alitoa Onyo Hilo Wakati Akiweka Wakfu Chuo Cha Biblia Kilichojengwa Kijiji Cha Sawee Mjini Babati.

Alisema; “Maaskofu Na Wachungaji Wote Wa TAG Wanaoandikisha Majina Yao Kwenye Ardhi Ya Kanisa Na Mali Zake Wanakosea Hao Ni Wezi Na Mafisadi Kwa Kuwa Mali Zote Za Kanisa Si Za Maaskofu Au Wachungaji”.

Aidha Alisema Kuandikisha Mali Za Kanisa Kwa Majina Ya Maaskofu Na Wachungaji Ni Kinyume Cha Sheria Za Nchi Na Kanisa Na Kufanya Hivyo Ni Hatari Sana Kwa Ustawi Wa Kanisa Ambalo Litakua Na Watu Wa Namna Hii.


Pia Alitoa Wito Huu Kwa Serikali; ” Natoa Wito Kwa Serikali Kupitia Kwa Miji, Manispaa Na Majiji Kabla Ya Kutoa Vibali Kwa Ajili Ya Mali Za Kanisa, Viandikishwe Kwa Majina Ya Taasisi Ambayo Ni Kanisa Na Si Waangalizi Wa Kanisa”.

Source; Nipashe.

Comments