RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI MTOTO: MUNGU AMENITUMA KUHUBIRI, SITAKI SADAKA – VIDEO




MTOTO Ibrahimu mwenye kipawa na karama ya aina yake ya kuhubiri, kuombea watu, na kuwaponya amesema kazi hiyo aliianza akiwa na umri wa miaka mitatu baada ya kuoteshwa na Mwenyezi Mungu na kumuita amtumikie.

Ibra akifanya mahojiano na Global TV Online amesema siku hiyo ilikuwa mchana akiwa amelala, ghafla aliota na kusikia sauti ya Mungu ikimuita na kumtaka akalihubiri neno la Mungu. Mtoto huyo ambaye kwa sasa anaoma Shule ya Msingi hapo kijijini kwao mkoani Arusha aliamka na kupanda kwenye mti kisha kuabnza kuhubiri

Haikukomea hapo tu, Ibra alijenga kibanda ambacho kila akitoka shule lazima afanye ibada ya maombi na mahubiri. Lakini siku moja kuna mlevi alipita na kukibomoa kibanda chake hicho cha mabati, kilichomkuta……….., Mungu ndo alitenda.

Ibra anaendelea kufunguka kwamba yeye hayuko kwa ajili ya sadaka kwani ametumwa na Mungu kuhubiri nakuponya wala si kuchukua sadaka za waumini. Anasema Mungu akimjalia atafungua kanisa lake kubwa ili kupanua wigo wa kutoa huduma hiyo ya maombi ambayo kwa sasa hufanya mpaka kwenye mahospitali.

MSIKIE MTOTO HUYO AKIFUNGUKA


Comments