RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JOYCE KIRIA AMKINGIA KIFUA MUNA


Joyce Kiria.

Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa kupitia Televisheni ya East Africa (EATV), Joyce Kiria amemkingia kifua muigizaji wa filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna’ kuwa yuko sahihi kwa hivi sasa anavyotoka na kuonekana kwenye mitandao kabla ya kumaliza 40 ya mtoto wake aliyefariki kwa sababu hana sababu ya kuendelea kulia na kujifungia ndani kama watu wanavyomtaka.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Kiria ambaye kwa sasa anasimamia kupinga ukatili kwa wanawake na kuwainua kiuchumi, alisema kwamba anachojua toka zamani Muna ni mzazi aliyempenda sana mtoto wake kupitiliza hivyo hata akitoka akiwa amevaa nini ni moja ya kujipa moyo na kuondoa machungu aliyonayo.

“Mimi binafsi nampongeza sana kwa kile anachokifanya sasa hivi, inaonekana jinsi gani alivyo shupavu maana bila hivyo basi angekuwa anaishi kwa maumivu makali tena ya kumsababishia athari ndani ya moyo,” alisema Kiria.

Mwanaharakati huyo leo pia atafanya semina yake kubwa kwa ajili ya kuwahamasisha wanawake waweze kujikwamua wenyewe ambayo itafanyika katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem

Comments