RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Nabii Brother Nicolaus Suguye amfanyia Maombi Mwita Waitara




Miongoni mwa Wabunge wawili waliojiunga na CCM hivi karibuni kutokea Vyama vya upinzani na sasa amechaguliwa na CCM kugombea tena Ubunge kwenye Jimbo hilohilo la UKONGA ambalo alikua Mbunge wake kupitia CHADEMA kabla ya kujiunga na CCM Ni Mh.Mwita Waitara

Wakati huu ambapo anajiandaa kuingia kwenye Uchaguzi wa marudio, Mwita amehudhuria ibada kwenye Kanisa la WRM Kivule Dar es salaam na kufanyiwa maombi na kiongozi wa Kanisa hilo Nicolaus Suguye

Kupitia Ukurasa Wake Nabii Brother Nicolaus Suguye ameandika;


“Mheshimiwa Mwita Waitara alipojumuika pamoja katika Ibada ya Kinabii inayoongozwa na Brother Nicolaus Suguye.Kheri viongozi wamtafutao Bwana kwamaana MUNGU ndie Mungu wa HAKI na mtoaji wa maarifa ya kweli.
-Brother Nicolaus Suguye”

Watu mbalimbali wamekua wakifika WRM kwa ajili ya maombi wakiwemo Viongozi wa Serikali na wa Kisiasa ambapo mwingine ambae alikwenda hivi karibuni ni Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye.

Furahia Upako Wa Picha Hapa chini




Comments