MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MITANDAO INASEMAJE JUU SAFARI YANGU YA SCOAN KWA TB JOSHUA

EMAILI YA REGINA MGAZA YA KUNIFARIJI NA KUNIPONGEZA

Regina Mgaza
5:12 asubuhi (Saa 8 zilizopita)

kwa mimi
Asante kwa kushukuru kwa kweli mimi nastahili kuitwa mama siyo dada, ninachoweza kusema ukweli Mungu akuwezeshe kupiga hatua zaidi kuliko ulipo sasa.
Nitajaribu kuwajuza wengine pia juu ya blogu yako. 

Mungu akupe kushinda katika kila hatua unayopitia na pia nimefurahishwa sana niliposoma juu ya mwaliko ulioupata toka kwa Nabii wa Mungu T B Joshua kwa kweli inanipasa kukupa hongera sana kwa kuwa wapo wanaofanya kazi zao vizuri lakini jiulize kwa nini Roho wa Mungu amwongoze kwako tu kwani wewe ni zaidi ya wengine? - Tafakari sana juu ya hili na mwambie Mungu asante, hiyo inatosha ninajua ulijifunza mengi sana ambayo kwa akili ya kibinadamu sio rahisi kuyajua na hasa ukizingatia tunamtumikia Mungu asiyeonekana na utendaji wake uko katika siri iliyoko moyoni mwake.  Isitoshe kumbe mtesi wako aliandaa ajali ya ndege ili usifikie kwenye kusudio la mwaliko wako, hakika ashukuriwe Mungu anayetulinda usiku na mchana bila hata sisi wenyewe kujua kinachoendelea.
Pia niliposoma historia ya maisha yako kwa kweli nilijisikia kuwa na huruma ambayo kibinadamu haisaidi ila kwa kuwa ni mama tena mjane sijui niseme nini, nilipoangalia tukio la msiba wa mama yako na jinsi ulivyokuwa umekuumiza sana ukweli basi acha nisiendelee, lakini furaha yangu kubwa ni kuwa yupo Mungu anayetufunika na faraja ya pekee napenda sana kusoma Zaburi 68:5. Ilikuwa siku moja nipo nyumbani nafuatilia kipindi cha Nabii TB Joshua akafundisha kupitia Zaburi hiyo, tangu siku hiyo nilibadilisha mwelekeo wa kuona niko pweke sina msaada wowote, lakini toka siku hiyo nilibadilisha mtazamo wangu na nilipojua kuwa Mungu ni baba wa yatima tena katika ujane wangu yeye ni mwamuzi wangu na inamalizia kuwa Mungu katika kao lake takatifu,  kila siku ninasikia kutiwa nguvu na kuwa na tumaini jipya kwa huyu Mungu asiyeonekana anayashangaza na kustajabisha sana.
Nisikuchoshe mwanangu kwa leo naiishia hapa.

Ilikuwa tarehe 23.05.2013 Saa 8 Mchana

-------------------------------------------------------------------------------------------------


UNCLE JIMMY AKITUPIA MASWALI KUHUSIANA NA SAFARI YANGU YA KWENDA SCOAN KWA NABII TB JOSHUA


Wakati flani niliwahi kuandika katika Makala zangu kazi ya Blogging ni wito tena wito hasa nasio kazi rahisi kama wengi wanavyodhani. Ni kama Mwandishi wa Habari wa Kujitegemea, unafanya kazi za watu zaidi ya watatu, unatafuta News, Unapiga Picha, Unaandika Story from the scratch, una I hariri habari kisha unaipaisha hewani.

It takes someones time and energy ndio maana bloggers wengi sana kazi inawashinda hasa unapokuwa hauna wito.

Ila unapoona kuna return ya kazi uliyoifanya kwenye maisha hasa kama hii ya uandishi ndipo unapopata moyo wa kuendelea. Ukiona mwenzio leo amepiga hatua badala ya kumponda unajipa moyo kuwa one day yes kama sio duniani basi mbinguni.

Tunatofautiana kwenye kutazama na ku rum blog, kwa sasa wengine tunatoka kwenye ku rum Blog sasa tunafikiria ku own a Media Company, maana kama unaweza Blog kwanini sio Gazeti, kama Sio Gazeti kwanini isiwe Magazine, kama unaweza kutengeneza interview na Popular Christian Artist kwanini Usitengeneze vipindi Vya TV, Blog is a stepping stone kwenye Christian Media Company.

Leo nina furaha sababu rafiki yangu blogger Rulea Sanga ambaye ni Graphic Artist Mzuri na anaye rum blog yake ya www.rumafrica.blogspot.com na ambaye ametengeneza Blog nyingi kwa kipindi kifupi ikiwemo ya Mcheza Filamu Vicent Kigosi a.k.a Ray na James Temu a.k.a Uncle Jimmy.

Mungu sio Mwakipesile Blogger anakwea Pipa Uso Kwa Uso SCOAN kuonana na Mtume TB Joshua jamaa akija lazima atakuwa na ma prophesy ya Kufufuka mtu.

Bloggers, Kushoto ni Rulea Sanga anayeenda Nigeria, Kulia ni Papaa Ze Bloger
Kutokana nakuvutiwa na Mtumishi wa Mungu huyo TB Joshua, Blogger Rulea Sanga ambaye kupitia Blog yake amekuwa akiandika makala mbalimbali zenye tabiri za Nabii TB Joshua. Mbali na Hilo Rulea katika Blog yake ameweka Picha nyingi za Nabii huyo nakufanya Blog yake kuwa kivutio kwa watu wanao mfahamu Mtumishi wa Mungu huyo "Just to see his face".

Fununu za Blogger huyu kupata mwaliko wa Mtumishi wa Mungu TB Joshua zilifungukia pand za Blog bila ajizi Blogger nikaruka hewani kongea Rulea.

Griiiiiiiiiiiiiii, Griiiiiiiiiiiiiii (Ndipo nikasema nilikuwa kijana na sasa ni mzee...caller tune)...Muito wa simu.

Blogger -Tumsifu Yesu Kristo!!habari za Mchana uko wapi blogger??

Rulea-Niko pande za Arusha, huku baridi si mchezo aiseee

Blogger- Kaka Kushangaa Baridi Arusha sawa sawa kushangaa Joto Dar-es-Salaam Arusha Kunani Kaka

Rulea-Hahahahaha, Kwa kweli, Arusha Niko na Glorious Celebration maeneo ya Unga limited

Blogger- Oooh, mie nakuja Next Week huko kuna Kitu cha FoF Kama kawaida, Kaka kuna jambo linawasha masikio yangu kuna tetesi kwenda kwa TB Joshua Nigeria kwa mwaliko wake mwenyewe Je ni kweli ama ndo danganya toto kula kunde mbichi?

Rulea-Kaka ni kweli nimepata mwaliko huo.Kaka kazi yetu ni nzito ila leo nafurahi sana kupata mwaliko huu kutokana na kazi hii ya Blog.

Blogger-Ilikuwaje mpaka akakupa mwaliko wa wewe kwenda Nigeria SCOAN.
Designer Rulea Sanga.


Rulea- Kusema za Ukweli kabisa namshanga Mungu sana.Ilikuwa siku moja nimekaa nyumbani nimepumzika baada ya shughuli za mwishoni mwa wiki, ghafla nikasikia simu yangu ikiita,nikapokea.Mtu niliyekuwa ninaongea nae alikuwa Mwanamke akaniuliza, kama mimi ndiye Rumaafrica-Nikamjibu ndio.Akasema tumefuraishwa na Blog yako na Nabii Tb Joshua amevutiwa na jinsi ulivyo weka picha zake na habari za kwake.

Blogger-Kwa kweli, ulijisikiaje baada ya kusikia hayo??

Rulea-Basi akaniambia niko na Nabii Tb Joshua Mwenyewe ongea nae online. Blogger huwezi amini,niliona kama muujiza kuongea na TB Joshua. Akanitia moyo kuwa hongera kwa kazi nzuri ya blog na ameipenda na anaomba anipe mwaliko kwenda Nigeria.

Blogger-Hapo hata mimi kaka nisingejiuliza mara 2 ama 3 kuwa ntakuja ama Sitakuja, Ni nini hasa kilicho mvutia Mtumishi wa Mungu katika Blog yako nampaka kupelekea yeye kukupa Mwaliko.

Rulea-Kikubwa hasa kilichomvutia ni mimi kuweka picha zake pale juu ya Blog yangu.Na amekuwa akifatilia habari ninazo ziandika zihusizo kanisa lake pamoja na Mungu anavyo mtumia.Ukiacha hayo mimi namkubali sana mtumishi wa Mungu huyu kwani amekuwa akifanya mambo makubwa duniani,amesaidia watu wengi duniani so kwangu ni furaha ilioje kwenda kukutana nae face to face.

Blogger-Mwaliko huu utakwenda peke yako kama Blogger au ametoa nafasi kwa watu wengine.
Emmanuel Mabisa anayeambatana na Rulea

Rulea-Amenipa Mwaliko wa mtu {1} hivyo nitakwenda na Emmanuel Mabisa Kiongozi wa Glorious Celebration Band

Blogger-Safari hii mnajigharamia wenyewe ama kuna Cost Sharing ama wao wana cover kila kitu.

Rulea- Wao ndio waliotuita Safari yote wamegharamia wa wenyewe nakumbuka nilipo maliza kuongea na TB Joshua alinirudisha kwa yule Dada nikaongea nae na akaniambia kwa hapa Tanzania Ofisi zao zipo Masaki, hivyo nitapokea details kutoka Masaki's Office.

Blogger-Hongera sana Rulea.Safari yetu itakuwa rasmi lini?

Rulea-Tunaondoka Tarehe 19/4/2012 siku ya Alhamisi yaani Kesho.

Blogger-Mnategemea kukaa siku ngapi.

Rulea-Kwa mujibu wa TB Joshua alisema ametupa Mwaliko wa wiki nzima.

Blogger-Mnatarajia kurudi lini Bongo land.

Rulea-tunatazamia any day from tarehe 26/27 ya mwezi huu.

Blogger-Rulea mimi sina mengi.Ila katuwakilishe vizuri kama Blogger wa Tz nakuombea safari njema.Usisahau zitendea kazi.

Rulea-Kaka nitakupa taarifa nikifika siku hiyo ila tuombeeni tufike salama.Mana kwa sasa Nigeria kuna vurugu.

Blogger -Tuko pamoja Kaka tutakuombea Mungu akufikishe salama.

Rulea-Amina Uncle

Blogger-Barikwa siku njema.

SOURCE:Story from www.unclejimmy.blogspot.com and www.samsasali.blogspot.com)Kazi Ya Blog Yampeleka Blogger Rulea Uso Kwa Uso na TB Joshua

------------------------------------------------------------------------------------------------

RUMAFRICA ILITUPIA YAFUATAYO KATIKA BLOGU YAKE

NDUNGU ZANGU NA WADAU WA BLOG HII, BLOGGER WENU RULEA SANGA NAPENDA KUWAAGA KWA KIPINDI CHA WIKI MOJA NITAKUWA NIGERIA KWA NABII TB JOSHUAMeneja Masoko Glorious Celebration na Blogger wa Blog hii, Rulea Sanga

Hatimaye safari yangu imefika ya kuelekea kwa Nabii TB Joshua. Safari yangu itaanza kesho saa 6:00 usiku siku ya Jumatano tarehe 18 Aprili 2012.

Mwaliko huu umetokana na Nabii TB Joshua kupendezewa na blog yangu ambayo mara nyingi huweka habari zake ambazo zimekuwa baraka kwa watu wengi ulimwenguni. Watu wengi wamekuwa wakinitumia "message na email" kuhusiana na wanavyobarikiwa na kazi ya mtumishi huyu.

Nakumbuka siku ya kwanza kupokea simu kutoka Nigeria, sikuamini maana ilikuwa ni muujiza kwangu. Nilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alijitambulisha kuwa yeye anatokea Nigeria kwa Nabii Joshua.....na mahojiano yetu yalikuwa kama ifuatavyo na yalifanyika kwa lugha ya kiingereza:

Simu: Dreeeeeeeeeee

Rulea: Nikaiangalia namba na kuona namba inatoka nje ya Tanzania....Nikaipokea simu.....Hellooo

Dada kutoka Nigeria: Hello....Habari yako.

Rulea: Salama, Habari yako.

Dada kutoka Nigeria:
Nzuri, napiga simu kutoka Nigeria kwa Nabii TB JoshuaRulea: (Nakahisi kutetetemeka) .... Ndiyo dada yangu unasemaje?

Dada kutoka Nigeria: Kuna habari fulani tumeziona katika blog yako zinazomhusu TB Joshua, ni wewe umeziweka na kuziandika?

Rulea: (Niliogopa sana nikidhani labda nimeandika kitu kibaya) ....Nikamwambia ni kweli nimeziandika ila zingine nimechukua katika blog za watu wengine..

Dada kutoka Nigeria: Sasa Nabii TB Joshua anataka kuongea na wewe

Rulea: (Mhhhh..akili yangu ikawa inawaza kuwa ni matepeli wa Nigeria) .... Ok sawa

Nabii TB Joshua: Hello...Habari yako.

Rulea: Nzuri, Bwana asifiwe?

Nabii TB Joshua: Ameni.....Nimependa kazi yako...natengependa nikualike SCOAN Nigeria....Natamani kukuona.

Rulea: Ahsante sana..mimi niko tayari katika mwaliko wako.

Nabii TB Joshua: Endelea kuongea na huyo dada uliyekuwa unaongea naye

Rulea: Nashukuru..Mungu akubariki

Dada kutoka Nigeria: Samahani..wewe ni nani katika kikundi cha Glorious Celebration, kwani tumeona katika blog yako na tumekipenda kwa huduma zake.?

Rulea: Mimi ni meneja masoko na pia ndiye ninayeweka habari zao katika mitandao

Dada kutoka Nigeria: Mko wangapi katika kikundi chenu?

Rulea:
Tupo kama watu kama 13

Dada kutoka Nigeria: Sasa si muda mrefu utapigiwa simu na "Cordinator" wetu aliyoko Tanzania, Dar es Salaam-Masaki anayeitwa Martha ili achukue habari zako na za kikundi cha Glorious Celebration.

Rulea: Sawa..nashukuru.

Dada kutoka Nigeria: Kwaheri ila tutakupigia tena

Baada ya muda mchache nikapokea simu kutoka kwa dada Martha aliyoko Tanzania.

Simu: Dreeeeeeeeee

Rulea: Hello

Martha: Habari yako...Ninaitwa Martha kutoka Masaki...ni cordinator wa kanisa la SCOAN Synagogue la Nabii TB Joshua wa Nigeria.

Rulea: Ndiyo dada yangu.

Martha: Umepokea simu yeyote kutoka Nigeria...

Rulea: Ndiyo:

Martha: Ninaomba kesho uje na baadhi ya viongozi wa Glorious Celebration Masaki.

Rulea: Sawa dada yangu nitafika.

Martha: Usiku mwema.

Rulea: Na wewe pia.

Baada ya muda mfupi nikainua simu yangu na kumpigia kiongozi wa muziki wa Glorious Celebration, Emmanuel Mabisa na kumwelekeza yaliyonikuta na kumweleza kesho tunatakiwa Masaki.

Siku ya pili ilipofika...tukafunga safari mpaka Masaki (walioenda ni Rulea, Emmanuel Mabisa na Chaka. Na tulipofika tukaulizwa maswali yanayohusiana na Historia fupi ya Glorious Celebration na uongozi wake. Na baada ya hapo kila mtu aliyefika mahali hapo akaanza kuulizwa "particulars" zake...na kila mtu akazitoa.

Baada ya kumaliza zoezi hilo tukaambiwa tutaitwa tena....Tulirudi majumbani kwetu na baada ya muda wa kama wiki moja hivi tukaitwa tena. Na kuelezwa ni watu wangapi wangeweza kwenda na vitu gani vya kufuata.....(Sitoweza kuelezea kila kitu mdau wangu)...Ila ningependa kukujulisha kwamba uongozi wa Nabii TB Joshua ulitoa namba ya watu kwenda nao...na ili-suggest kumchukua kiongozi mmoja wa Glorious Celebration, Emmanuel Mabisa kama muwakilishi wa kikundi

Kwa kumalizia tu, baada ya muda wa miezi miwili nikimaanisha Februali-Aprili niliitwa na dada Martha katika ofisi zao zilizoko Posta katika jengo la Benjamini Mkapa floor ya kwanza na kupewa fomu za kujaza kwaajili ya VISA. Nakumbuka kipindi kilikuwa kigumu sana kwangu kwani rafiki yangu Emmanuel Mabisa alikuwa katika maombi Chanika na Glorious Celebratoion kwaajili ya maandalizi ya Pasaka. Na nilipompigia simu kuwa wanahitaji passport yako..na yeye akasema yuko mbali na hataweza kufika kwa siku hiyo, na akaniamuru nibomoe ofisi yake na kutafuta hiyo passport..na mimi nilifanya hivyo.

Zoezi la ujazaji form lilipoisha niliambiwa nitapigiwa simu kujua siku ya kuondoka kuelekea Nigeria. Sikumbuki ni tarehe ngapi ila ni mwezi wa April nikatumiwa message ikinijulisha kuwa tarehe 8 April 2012 tunatakiwa kwenda ofisi za TB Joshua kwaajili ya maelekezo ya safari. Jumatatu 16 April nikiwa Arusha katika Uzinduzi wa Albamu ya Ruach Waorship Team nikatumiwa message kuwa tarehe 17 April natakiwa asubuhi kuwa katika ofisi za TB Joshua-Tanzania kupewa maelekezo ya safari ya tarehe 18...na mimi nilimjibu kuwa itakuwa ngumu kufika kwani hiyo tarehe ndiyo tarehe ambayo nitakuwa natoka Arusha kwahiyo nikifika Dar es Salaam nitakufuata....Na dada Martha akanijibu kuwa basi tutaonana Airport saa sita usiku

Hayo ndiyo maelezo ya safari yetu ya kulelea kwa Nabii TB Joshua..Na sasa tunasubiria kuondoka 18 Aprili usiku wa saa sita

TUNAOMBA MAOMBEZI YAKO TUFIKE SALAMA NA TURUDI SALAMA


1