Mkurugenzi wa Rumafrica For All Nations aliweza kuandika story fupi ya safari yake ya kuelekea Nigeria alikoalikwa na Nabii TB Joshua baada ya kuguswa na huduma yake habari za mitandaoni, na hivi ndivyo alivyoandika kwa wadau wake wa Rumafrica For All Nations.
"Hatimaye safari yangu imefika ya kuelekea kwa Nabii TB Joshua. Safari yangu itaanza kesho saa 6:00 usiku siku ya Jumatano tarehe 18 Aprili 2012.Mwaliko huu umetokana na Nabii TB Joshua kuvutiwa na blog yangu ya RUMAFRICA ambayo mara nyingi huweka habari mbalimbali za Injili pamoja na huduma ya SCOAN, na habari hizi zimefanyika baraka kwa watu wengi ulimwenguni. Watu wengi wamekuwa wakinitumia "message na email" kuhusiana na wanavyobarikiwa na kazi yangu hii ya mitandaoni.
Nikiwa nyumbani kwangu Sinza kwa Remy jijini Dar es Salaam nilisikia simu ikiita nikiwa sebuleni, na nilipoangalia niliona namba za nje ya Tanzania, nilipokea ile simu nikijua ni wadau wangu wananipigia kujua zaidi kuhusu post zangu. Nilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alijitambulisha kuwa yeye anatokea Nigeria kwa Nabii TB Joshua, na mahojiano yetu yalikuwa kama ifuatavyo na yalifanyika kwa lugha ya Kiingereza:
Simu: Dreeeeeeeeeee
Rulea: Nikaiangalia namba na kuona namba inatoka nje ya Tanzania....Nikaipokea simu.....Hellooo
Dada kutoka Nigeria: Hello....Habari yako.
Rulea: Salama, Habari yako.
Dada kutoka Nigeria: Nzuri, napiga simu kutoka Nigeria kwa Nabii TB Joshua
Rulea: (Nakahisi kutetetemeka) .... Ndiyo dada yangu unasemaje?
Dada kutoka Nigeria: Kuna habari fulani tumeziona katika blogu yako zinazomhusu TB Joshua, ni wewe umeziweka na kuziandika?
Rulea: (Niliogopa sana nikidhani labda nimeandika kitu kibaya) ....Nikamwambia ni kweli nimeziandika ila zingine nimechukua katika blogu za watu wengine..
Dada kutoka Nigeria: Sasa Nabii TB Joshua anataka kuongea na wewe, upo tayari
Rulea: (Nikasita...Mhhhh..akili yangu ikawa inawaza kuwa ni matepeli wa Nigeria) .... Ok sawa.
Nabii TB Joshua: Hello...Habari yako.
Rulea: Nzuri, Bwana asifiwe?
Nabii TB Joshua: Ameni.....Nimependa kazi yako...ningependa nikualike SCOAN Nigeria....Natamani kukuona.
Rulea: Ahsante sana..mimi niko tayari kwa mwaliko wako.
Nabii TB Joshua: Endelea kuongea na huyo dada uliyekuwa unaongea naye, akuunganishe na Cordinator wetu aliyoko huko Tanzania, Dar es Salaam
Rulea: Nashukuru..Mungu akubariki
Dada kutoka Nigeria: Samahani..wewe ni nani katika kikundi cha Glorious Celebration? Kwani tumeona katika blog yako na tumekipenda kikundi chenu.
Rulea: Mimi ni meneja masoko na ni mmoja wa waanzilishi wa kikundi hiki na pia ndiye ninayeweka habari za kikundi katika mitandao mbalimbali.
Dada kutoka Nigeria: Mko wangapi katika kikundi chenu?
Rulea: Tupo kama watu kama 13
Dada kutoka Nigeria: Sasa si muda mrefu utapigiwa simu na "Cordinator" wetu aliyoko Tanzania, Dar es Salaam-Masaki anayeitwa Martha ili achukue habari zako na za kikundi cha Glorious Celebration. Pia ningeomba utakapokuwa unakuja Nigeria uongozane kikundi chako cha Glorious ila watu kama saba tu wanatosha na tutamwambia Martha
Rulea: Sawa..nashukuru.
Dada kutoka Nigeria: Kwaheri ila tutakupigia tena.
Simu ikakatwa. Jamani nilikuwa na amani ndani ya mtima wangu, nilijawa na furaha ya ajabu sana isiyoelezeka.
Baada ya muda mchache nikapokea simu kutoka kwa dada Martha kutoka Masaki, Dar es Salaam Tanzania.
Simu: Dreeeeeeeeee
Rulea: Hello
Martha: Habari yako...Ninaitwa Martha kutoka Masaki...ni cordinator wa kanisa la SCOAN Synagogue la Nabii TB Joshua wa Nigeria.
Rulea: Ndiyo dada yangu.
Martha: Umepokea simu yeyote kutoka Nigeria...
Rulea: Ndiyo
Martha: Samahani ningependa kujua ni kitu gani umefanya mpaka Nabii TB Joshua kukupigia wewe, maana hata sisi huwa hatupigii simu mara kwa mara, mara nyingi watu wake ndio wanaokuwa wakitupigia. Please naomba uniambia maana siamini kabisa kuona Nabii TB Joshua ameweza kukupigia simu wewe na kunisisitiza sana niwasiliane na wewe.
Rulea: Mhh dada yangu, hata mimi naona ni muujiza wa ajabu. Ila kwa ufupi ni kwamba amenipigia baada ya kuvutiwa na kazi zangu za mitandaoni kuhusu huduma yake.
Martha: Kwa kweli umemgusa sana, na una bahati ya pekee sana. Mimi naomba nikupongeze .
Rulea: Asante sana dada yangu
Martha: Ninaomba kesho uje na baadhi ya viongozi wa Glorious Celebration Masaki.
Rulea: Sawa dada yangu nitafika.
Martha: Usiku mwema.
Rulea: Na wewe pia.
Baada ya muda mfupi nikainua simu yangu na kumpigia kiongozi wa muziki wa Glorious Celebration, Emmanuel Mabisa na kumwelekeza yaliyonikuta na kumweleza kesho tunatakiwa Masaki kumuona Martha.
Siku ya pili ilipofika...tukafunga safari mpaka Masaki (tulioenda ni Rulea, Emmanuel Mabisa na Chaka. Na tulipofika tukaulizwa maswali yanayohusiana na Historia fupi ya Glorious Celebration na uongozi wake. Na baada ya hapo kila mtu akuulizwa "particulars" zake...na kila mtu akazitoa.
Baada ya kumaliza zoezi hilo tukaambiwa tutaitwa tena....Tulirudi majumbani kwetu na baada ya muda wa kama wiki moja hivi tukaitwa tena Masaki kwa Martha.
Tulipofika Masaki, Martha akatuuliza ni watu wangapi kutoka kwenye kikundi wangependa kwenda Nigeria.
(Sitoweza kuelezea kila kitu mdau wangu tulichoongea na Martha kwasababu mengine ni mambo ya mtu binafsi)...Ila ningependa kukujulisha kwamba uongozi wa Nabii TB Joshua alitoa namba ya watu kwenda nao ni kama watu saba 7.
Sasa baada ya kumaliza maongezi na Martha tuliruhusiwa kwenda nyumbani, na kuambiwa kuwa Martha mwenyewe atatupigia siku kurudi tena kwaajili ya kujaza fomu kwaajili ya safari ya Nigeria.
Baada ya wiki kama mbili hivi Martha akanipigia simu kwenda ofisini kwake Masaki na Emmanuel Mabisa. Tulipofika pale tuliongea mengi ila la msingi ni kwamba, Martha aliweza kutuambia kuwa watu wanaohitajika kwenda ni watu wanne na sio saba tena kama Nabii TB Joshua alivyotuambia. Tulipoambiwa hivyo tulikubali. Martha akatuomba tuchague watu wa kwenda Nigeria. Tuliweza kumchagua Angel Bernard, Emmanuel Mabisa, Chaka na mimi Rulea Sanga. Baada ha yapo tuliruhusiwa kwenda nyumbani.
Zilipita wiki kadhaa, nikampigia simu Martha kumkumbusha juu ya safari maana niliona kimia sana. Martha alinipangia siku ya kuonana naye. Ilipofika siku ya kuonana alinipigia simu nienda katika ofisi za Nabii TB Joshua zilizopo katika Jengo la Benjamini Floor ya chini, jijini Dar es Salaam. Nilipofika pale akanambia kuwa Nabii TB Joshua amepunguza tena watu wa kwenda Nigeria, kwahiyo wataenda watu wawili yaani Rulea Sanga na Emmanuel Mabisa. Nilikubaliana naye, na yeye akanipangia siku ya kuonana naye.
Baada ya muda wa miezi miwili nikimaanisha kuanzia Februali hadi Aprili niliitwa na dada Martha katika ofisi zao zilizoko Posta katika jengo la Benjamini Mkapa floor ya kwanza na kupewa fomu za kujaza kwaajili ya VISA. Nakumbuka kipindi kilikuwa kigumu sana kwangu kwani rafiki yangu Emmanuel Mabisa alikuwa katika maombi Chanika na Glorious Celebratoion kwaajili ya maandalizi ya Pasaka. Na nilipompigia simu kuwa wanahitaji passport yake, akasema yuko mbali na hataweza kufika kwa siku hiyo, na akaniamuru nibomoe mlango wa ofisi yake iliyokuwa Afrikasana Sinza ili kutafuta hiyo passport..na mimi nilifanya hivyo.
Zoezi la ujazaji form lilipoisha niliambiwa tutapigiwa simu kujua siku ya kuondoka na kuelekea Nigeria. Sikumbuki ni tarehe ngapi ila ni mwezi wa April nikatumiwa message ikinijulisha kuwa tarehe 8 April 2012 tunatakiwa kwenda ofisi za Nabii TB Joshua kwaajili ya maelekezo ya safari. Jumatatu 16 April nikiwa Arusha katika Uzinduzi wa Albamu ya Ruach Waorship Team nikatumiwa message kuwa tarehe 17 April natakiwa asubuhi kuwa katika ofisi za Nabii TB Joshua Dar es Salaam-Tanzania kupewa maelekezo ya safari ya tarehe 18...na mimi nilimjibu kuwa itakuwa ngumu kufika kwani hiyo tarehe ndiyo tarehe ambayo nitakuwa natoka Arusha kwahiyo nikamwambia nikifika Dar es Salaam nitamfuata....Na dada Martha akanijibu kuwa basi tutaonana Airport saa sita usiku.
Nilipofika Dar es Salaam, maandalizi yalifanyika kwa haraka sana na mida ya saa 3 usiku mimi na Emmanuel Mabisa tulifika airport na kumkuta Martha akiwa na watu wengine wanaoelekea kwa Nabii TB Joshua.
Hayo ndiyo maelezo ya safari yetu ya kulelea kwa Nabii TB Joshua..Na sasa tunasubiria kuondoka 18 Aprili usiku wa saa sita
SASA BONYEZA HAPA KUONA SAFARI YETU KUTOKA DAR ES SALAAM, ETHIOPIA NA HATIMAYE NIGERIA KWA NABII TB JOSHUA