RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KAMA WEWE HUTAMBARIKI PASCAL CASSIAN MSHINDI WA BSS 2009 KWA KUNUNUA CD YAKE YA "WASAMEHE BURE", WAPO WATAKAO NUNUA AMBAO MUNGU ANAWAPENDA.

Mwandishi: Rulea Sanga

Mungu ana watu wake ambao anatumia kwaajili ya kazi yake. Wewe kama hupendi kufanya kazi ya Mungu wapo ambao watafanya kazi YAKE, kwahiyo dharau zako na majivuno yako hayasaidi chochote machoni pa Mungu. Kuna watu wanalia kila siku ili wamtumikie Mungu, wewe sio peke yako unaweza kumpendeza Mungu. Utajivuna sana lakini kwa Mungu unaonekana kama uchafu na siku ya mwisho MUNGU atakutema na kukutapika.

Nikiwa katika eneo la chakula SCOAN. Bonyeza hapa kuona nilipokuwa huko kwa neema ya Mungu:
http://rumaafrica.blogspot.com/p/tb-joshua-invited-rulea-sanga-and.html

Mungu ni mwenye huruma sana, kama wewe umeshatambua kuwa katika maisha yako umekuwa sio msaada kwa Mungu, leo unaweza kumgeuza Mungu shingo yake na sura yake ikaaangalia kwako. Kumgeuza Mungu kunafanyika kwa kutubu dhambi zako na kuanza maisha mengine mapya ya kumtumikia Mungu.

Mungu hajakunyima kipaji, katika mwili wako kuna vitu vingi unaweza kufanya kwaajili ya Mungu.
Pascal Cassian alitambua hilo na kuona kuamua kufanya mambo ya Mungu na kuachana na ya dunia baada ya kuona hayatamsaidia lolote. Ukiwa na nia h kufanya jambo hata kama huna uwezo wa kufanya, Mungu hutumia watu wake kukuwezesha wewe kufanya lile ambalo umekusujudia kwa utukufu wake. Pascal Cassian alikuwa anauwezo wa kuimba lakini alikuwa anashindwa atawaaimbia watu gani na watu kuona kile ambacho Mungu amempatia. Mungu akaamua kumtumia Mkurugenzi wa BSS, Madam Ritha na kumuwezesha kutambua kile alichokuwa nacho Pascal Cassian na kushirikisha katika mashindo ya BSS 2009. Mungu hakuweza kumuabisha Pascal Cassian na Mdam Ritha. Mungu alimpa uwezo mkubwa wakuimba vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa BSS 2009.

Baada ya ushindi huo, Pascal Cassian aliamua kutulia kidogo kumsikiliza Mungu nini cha kufanya baada ya ushindi wake. Ndipo alipoaamua kutoa albamu yake ya "WASAMEHE BURE". Kuna maneno yameimbwa katika CD hiyo ambayo yatakufanya upende na kuelimika kwa njia moja au nyingine.

Kutoka na hekima aliyonayo Pascal Cassian, aliamua kuweka picha ya Madam Ritha katika cover la CD yake kuonyesha kuwa Mungu anaweza kumtumia mtu "from no way" na kukuinua, kwahiyo tunaweza kusema Mungu hawezi kuonekana LIVE na kukupa mafanikio ila anaonekana kwa kupitia viumbe vyake alivyoviumba.

Ruma Africa inakupa uamuzi wako wa kuamua kumuunga mkono Pascal Cassian kwa kununua CD yake au kutonunua.
Kama hutanunua wapo ambao watanunua, 
Kama wewe hutamuunga mkono wapo watakao muunga mkono, 
Kama wewe hutambariki wapo watakaombariki, 
Kama wewe hutamuweza kumpa riziki yake kwa kupitia huduma yake, wapo watakaompa riziki.
Kama wewe unafikiria hasi, wapo wanafikiria chanya kwa mafanikio ya Pascal Cassian

Mungu akuwezeshe kutoa uamuzi wako mzuri kwaajili ya kazi ya Mungu kwa kupiatia Pascal Cassian





Hizi ndizo nyimbo zinazopatikana katika Albamu yake hii.

Comments