MATUKIO YA TAMASHA LA MARY MGOGO KATIKA UZINDUZI WA DVD YAKE YA MUNGU WA AJABU NDANI YA UBUNGO PLAZA
Mary Mgogo ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Muimbaji huyu ameokoka akiwa mdogo na anazidi kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Ni Mtanzania na mzalendo, anapenda sana kumtumikia Mungu kwa kupitia vipaji alivyopewa ikiwa pamoja na uimbaji.
Siku ya Jumapili 5/07/2015 aliweza kuzindua DVD yake ya Mungu wa ajabu ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza. Mgeni Rasmi alikuwa ni Mh. Makongoro Mahanga, Mbunge wa Segerea DSM na Naibu Waziri wa Ajira na Kazi.
Tamasha hili liliwakusanya waimbaji mbalimbali kama vile Atosha Kissava, Tumaini Njole, Eno na Edo, Mess Chengula, Christina Mbilinyi, Ibrahim Sanga, Edson Mwasabwite, Bahati Bukuku, Leah Mwankundile, Veneranda Bugeraha, Double J (Jesca na Judy) na wengine wengi kama utakavyowaona katika picha.
Rumafrica ilihusika katika upambaji wa ukumbi, video na still picture. Unaweza kutembele www.rumafrica.blogspot.com kujua mengi zaidi au tupigie +255 715 851 523.
TUONE MARY MGOGO AKIWA KATIKA CHUMBA CHA VIP NA DANCERS WAKE KABLA YA KUINGIA UKUMBINI
TUONE MARY MGOGO AKIWA KATIKA CHUMBA CHA VIP NA DANCERS WAKE KABLA YA KUINGIA UKUMBINI
Kulia ni Mary Mgogo
Kulia ni mtoto wa kwanza wa Mary Mgogo
Mary Mgogo akiwa na dancers wake Edo na Eno (kushoto)
Mary Mgogo (kushoto) na mwanae wa kwanza
Comments